Appeal for Peace by new UN Secretary-General António Guterres

Back to News and Events

Appeal for Peace by new UN Secretary-General António Guterres

(In both English and Kiswahili)

(New York, 01 Jan 2017). On my first day as Secretary-General of the United Nations, one question weighs heavily on my heart.

How can we help the millions of people caught up in conflict, suffering massively in wars with no end in sight?

Civilians are pounded with deadly force. Women, children and men are killed and injured, forced from their homes, dispossessed and destitute. Even hospitals and aid convoys are targeted.

No one wins these wars; everyone loses. Trillions of dollars are spent destroying societies and economies, fueling cycles of mistrust and fear that can last for generations. Whole regions are destabilized and the new threat of global terrorism affects us all.

On this New Year’s Day, I ask all of you to join me in making one shared New Year’s resolution:
Let us resolve to put peace first.
Let us make 2017 a year in which we all – citizens, governments, leaders – strive to overcome our differences.

From solidarity and compassion in our daily lives, to dialogue and respect across political divides… From ceasefires on the battlefield, to compromise at the negotiating table to reach political solutions…

Peace must be our goal and our guide.

All that we strive for as a human family – dignity and hope, progress and prosperity – depends on peace.

But peace depends on us.

I appeal to you all to join me in committing to peace, today and every day.

Let us make 2017 a year for peace.

Thank you.

======================================

( New York, 01 Jan 2017). Katika siku yangu ya kwanza kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, moyo wangu umegubikwa na swali moja.

Je tunaweza vipi kusaidia mamilioni ya watu walionasa kwenye mizozo, wakikumbwa na machungu mengi kwenye vita visivyo na dalili za kumalizika?

Makombora mazito yanaangukia raia. Wanawake, watoto na wanaume wanauawa na wanajeruhiwa, wakilazimika kukimbia makwao, bila mali zao na kusalia hohehahe. Hata hospitali na misafara inalengwa.

Hakuna mshindi kwenye vita hivi; kila mtu anapata hasara. Trilioni za dola zinatumika kuharibu jamii na uchumi na kuchochea mzunguko wa kutokuaminiana na hofu, mambo yanayoweza kudumu vizazi na vizazi. Maeneo yyote yamekosa utulivu na kitisho kipya ya ugaidi duniani kinatuathiri sote.

Katika siku hii ya mwaka mpya, nawasihi nyote muungane nami kuweka azimio la pamoja la mwaka mpya:

Hebu na tuazimie kuweka mbele amani.

Hebu na tuufanye mwaka 2017, uwe mwaka ambao kwao sisi sote, raia, serikali, viongozi tunahangaika kumaliza tofauti zetu.

Kuanzia mshikamano na upendo kwenye maisha yetu ya kila siku hadi mazungumzo na kuheshimiana katika migawanyiko yetu ya kisiasa….

Kuanzia kusitisha mapigano kwenye maeneo ya vita hadi kulegeza misimamo kwenye meza za mazungumzo na kufikia suluhu ya kisiasa.

Amani lazima iwe lengo na mwongozo wetu.

Yote yale ambayo tunahangaika kama familia ya kibinadamu – utu na matumaini, maendeleo na ustawi- yanategemea amani.

Lakini amani inatugemea sisi.

Nawasihi nyote muungane nami kuazimia amani, leo na siku zote.

Hebu na tuufanye mwaka 2017 uwe mwaka wa amani.

Asanteni.

Back to News and Events