SWAHILI
|
 |
Nchi zote 189 wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeahidi kutekeleza yafuatayo ifikapo mwaka 2015:
- Kutokomeza umasikini uliokithiri na njaa
- Kupunguza kwa asilimia 50 idadi ya watu masikini ambao kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku
- Kupunguza kwa asilimia hamsini idadi ya watu wanaokumbwa na njaa
- Elimu ya msingi kwa wote
- Kuhakikisha watoto wote wa kike na wa kiume wanahitimu elimu ya shule ya msingi
- Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa wanawake
- Kuondoa tofauti ya uwiano wa wasichana na wavulana katika elimu ya msingi ifikapo mwaka 2002, na katika ngazi zote za elimu ifikapo 2015
- Kupunguza vifo vya watoto wachanga
- Kupunguza kwa theluthi mbili vifo vya watoto wa umri chini ya miaka mitano
- Upatikanaji wa huduma bora za uzazi
- Kupunguza kwa robo tatu idadi ya vifo vya uzazi
- Kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine
- Kuzuia kabisa na kuanza kupunguza maambukizo mapya ya ukimwi
- Kuzuia kabisa na kuanza kupunguza milipuko ya malaria na magonjwa mengine hatari
- Kulinda mazingira yetu
- Kujumuisha misingi yote ya maendeleo endelevu katika sera na programu za kila nchi; kuzuia upotevu wa rasilimali ya mazingira
- Kupunguza kwa silimia 50 idadi ya watu wanaoshindwa kupata maji safi na salama
- Kutimiza lengo letu la kuboresha maisha ya watu wapatao angalau milioni 100 wanaoishi mijini katika makazi yasiyo na hadhi ifikapo mwaka 2020
- Kujenga mshikamano wa kimaendeleo duniani
- Kuboreha zaidi mfumo wa fedha na biashara duniani kuhakikisha unakuwa wa usawa, unafuata sheria na kamwe hauwi wa kibaguzi. Mataifa yote yatekeleze dhana ya utawala bora na yashirikiane kuleta maendeleo na kupunguza umasikini—ndani ya nchi zao na kimataifa
- Kushughulikia mahitaji ya kipekee ya nchi changa. Hii ni pamoja na
kuondoa ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi changa;
kutekeleza mpango wa kuzipunguzia madeni nchi masikini kabisa duniani zenye madeni makubwa; kuzifutia kabisa madeni wanayodaiwa na nchi moja moja zilizoendelea; kutoa misaada zaidi kwa nchi masikini ambazo zinaonyesha jitihada za kutumia misaada hiyo katika kuondoa umasikini
- Kushughulikia suala la mahitaji muhimu ya visiwa vidogo na nchi zisizo na bandari ambazo ni miongoni mwa nchi zinazoendelea
- Kushughulikia ipasavyo kwa kutumia vyombo vya kitaifa na kimataifa suala la madeni yanayozikabili nchi zinazoendelea ili kuziwezesha nchi hizo ziweze kulipa madeni yao
- Kwa kushirikiana na nchi zinazoendelea, kuweka utaratibu wa kuwapatia vijana ajira bora
- Kwa kushirikiana na kampuni zinazotengeneza madawa, kuwezesha nchi zinazoendelea kupata dawa muhimu kwa bei nafuu
- Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuwezesha nchi zinazoendelea kutumia teknolojia ya kisasa, hasa katika nyanja ya habari na mawasiliano
Kwa habari zaidi kuhusu Malengo ya Maendeleo ya Milenia tazama katika tovuti ya Umoja wa Mataifa www.un.org/millenniumgoals.
Imechapishwa na Idara ya Habari ya Umoja wa Mataifa
New York, DPI/2263---Februari 2002—30M.
Imetafsiriwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa,
Dar es Salaam |